ASKARI WA JWTZ ADAIWA KUJIUA KWA KUJIRUSHA BAHARINI AKISAFIRI NA BOTI | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, October 6, 2018

ASKARI WA JWTZ ADAIWA KUJIUA KWA KUJIRUSHA BAHARINI AKISAFIRI NA BOTI

  Malunde       Saturday, October 6, 2018
Askari  wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), amefariki dunia baada ya kujirusha baharini akisafiri na boti ya Azam.

Kifo cha askari huyo ni moja ya matukio matatu ya watu waliojitupa baharini wakiwa safarini kwa kutumia usafiri huo, akiwamo mtoto aliyeokolewa akiwa hai.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Azam Marine, Abubakar Aziz, alisema jana kuwa askari huyo alifariki dunia hivi karibuni na kwamba hayo ni miongoni mwa matukio ambayo yamewahi kujitokeza katika boti zao.

Aziz alisema katika matukio hayo, watu wawili akiwemo mwanajeshi huyo walijitosa baharini wakati meli ikiendelea na safari na askari huyo alijitosa eneo lenye kina kirefu kiasi kwamba asingeweza kuokolewa.

"Matukio haya yalitokea kwa nyakati tofauti ambapo baada ya kujitupa baharini licha ya juhudi kufanyika za kuwatafuta, hatukuwapata. Walipatikana siku nne baadaye akiwa tayari wameshafariki dunia," alisema.

Credit: Nipashe
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post