BOSI WA TAKUKURU DIWANI ATHUMANI AKABIDHI OFISI YA KATIBU TAWALA MKOA WA KAGERA


Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Nchini Kamishina wa Polisi Diwani Athumani akiagana na mkuu wa mkoa wa Kagera brigedia jenerali Marco Gaguti katika ukumbi wa mikutano wa halmshauri ya Bukoba leo Oktoba 1,2018.Picha na Agela Sebastian - Malunde1 blog


****
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Nchini Kamishina wa Polisi Diwani Athumani amekabidhi ofisi ya katibu tawala katika mkoa wa Kagera ambayo alikuwa akiitumikia kwa takribani miaka miwili kabla ya kuteuliwa kuwa mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU.

Akiagana na watumishi wa kada mbalimbali mkoani Kagera leo Oktoba 1,2018 pia ameweka wazi mikakati yake ya muda mfupi,kati na mrefu itakayowezesha TAKUKURU kuendelea kuaminiwa na wananchi wa taifa la Tanzania.

Kiongozi huyo mkuu wa TAKUKURU amesema nafasi hiyo imetokana na ushirikiano kati ya watumishi pamoja na wanakagera na hatimaye kumfanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kumuamini na kumteua aongoze TAKUKURU.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post