Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Tekonolojia (COSTECH), Dkt. Amos Nungu, akimkabidhi cheti, Mwandishi wa Habari Suleiman Msuya, baada ya kushiriki mafunzo ya kuandika habari za Teknolojia ya Uhandisi Jeni (GMO), yaliyofanyika New Dodoma Hoteli mkoani Dodoma Oktoba 17,2018 na kuibuka Mshindi wa Pili katika Mashindano ya uandishi wa habari juu ya teknolojia hiyo kwa kundi la Waandishi wa habari za magazeti. Mafunzo hayo yaliandaliwa na Jukwaa la Wazi la Kilimo na Teknolojia Afrika (OFAB) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Cornell cha Marekani, Cornell Alliance For Science na African Agricutural Technology Foundation (AATF).
Mshindi wa kwanza wa kuandika habari hizo kwa njia ya redio katika mafunzo hayo, Kemsi Fadhil akipokea cheti.
Mshindi wa pili wa kuandika habari za GMO kwa njia ya Televisheni, Vumilia Kondo akipokea cheti.
Mshindi wa kwanza wa kuandika habari za GMO kwa njia ya Televisheni katika mafunzo hayo, Doreen Mlay akipokea cheti.
Meza kuu wakati wa utoaji wa vyeti hivyo.
Mshindi wa jumla wa kuandika habari za GMO kwa njia ya magazeti katika mafunzo hayo, Rose Milondo akikabidhiwa cheti.
Mwanahabari Dotto Mwaibale akipokea cheti cha ushiriki.
Picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo.