AJALI YA MV NYERERE YAMHAMISHIA CCM MBUNGE WA CHADEMA UKEREWE

Mbunge wa Ukerewe, Joseph Michael Mkundi ametangaza kujiuzulu uanachama na nyadhifa zake zote ndani ya CHADEMA, na kuomba kujiunga CCM.

Miongoni mwa sababu alizotoa, ni kutopata ushirikiano kutoka kwa viongozi wenzake (CHADEMA) wakati wa ajali ya MV Nyerere.

"Chama cha Siasa kama Taasisi ya Umma na inayotoa maelekezo Kwetu wawakilishi wa Wananchi, yenyewe inapokuwa msingi wa Kujenga Chuki, uhasama, ubaguzi na Ukinzani na serikali. Taasisi hii inapoteza Uhalali wa Kiuongozi (leadership Legitimacy).

"Kwa Msingi Huo Leo Siku ya Jumatano tarehe 10 Oktoba 2018 natangaza kujivua uanachama wa Chadema na hii ikiwa kwa Mujibu wa Katiba ya Chadema ibara ya 5.4.1,chama ambacho kwa Tiketi yake nilikuwa Diwani wa Kata ya Bukiko na Mbunge wa Jimbo la Ukerewe

"Natangaza kuomba Kujiunga na CCM, Chama ambacho kwa hakika nimeona wakidhihirisha kwa Vitendo Itikadi yao ambayo imejengwa katika misingi ya Utu, Undugu, Mshikamano, Haki na Umoja wa watu wa Tanzania" -Joseph Michael Mkundi 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post