Picha : AJALI YA GARI YA WIZARA YA KILIMO YAUA WATUMISHI WATANO MANYONI


Watu watano wanadaiwa kupoteza maisha katika ajali ya Gari ndogo, ya Wizara ya Kilimo iliyokuwa imebeba wataalamu wanne pamoja na dereva wote wamefariki papo hapo katika eneo la Njirii Manyoni mkoani Singida leo Jumapili Oktoba 21,2018
.

  Inaelezwa kuwa wanaume ni watatu na wanawake wawili. 

TANZIA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo anapenda kuwataarifu ya kuwa Wizara ya Kilimo imepatwa na msiba wa Watumishi wake Watano (5) waliopata ajali leo asubuhi tarehe 21 Oktoba, 2018 Manyoni mkoani Singida, walipokuwa safarini kuelekea Mwanza kikazi.

 Watumishi hao waliofariki ni;
1. Stella Joram Ossano (39)
2. Esta Tadayo Mutatembwa (36)
3. Abdallah Selemani Mushumbusi (53)
4. Charles Josephat Somi
5. Erasto Mhina (43)

Miili ya marehemu ipo njiani kuja Hospitali ya Mkoa wa Dodoma leo tarehe 21 Oktoba 2018.


Mungu azilaze roho zao mahala pema peponi, Amina🙏🏿

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527