IDADI YA WALIOFARIKI KWENYE KIVUKO YAFIKIA 196Saa 7:28 Septemba 22,2018

Idadi ya watu walioopolewa ziwani yafikia 196 zoezi la uopoaji na uokoaji linaendelea.


Saa 5:22 Asubuhi Septemba 22

Mhandisi wa Kivuko cha Mv.Nyerere kilichopata ajali ya kuzama ziwa Victoria .Alphonce Charahani ameokolewa muda mfupi uliopita akiwa hai japo hali yake ni mbaya lakini anapatiwa huduma.

Imeelezwa fundi huyo alikuwa amekwama kwenye moja ya vyumba vya manahodha na alikuwa akigongagonga vitu ili waokoaji wamsikie jambo ambalo limetimia.

Lakini hawezi kuongea kutokana na hali yake kuwa mbaya baada ya kukaa ndani ya maji kwa takribani siku tatu.

Theme images by rion819. Powered by Blogger.