SERIKALI YASEMA JUMATATU NI SIKU YA KAZI KAMA KAWAIDA.... RAIS ALITANGAZA MAOMBOLEZO, SIO MAPUMZIKO


Serikali kupitia kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa imetoa ufafanuzi kuwa Jumatatu Septemba 24, 2018 ni siku ya kazi kama kawaida.

Baada ya Rais Magufuli kutangaza siku 4 za maombolezo kufuatia ajali ya MV Nyerere iliyoua watu zaidi ya 190 mpaka sasa, kumekuwa na mkanganyiko kidogo kwa baadhi ya watu kudhani Jumatatu itakuwa ni mapumziko.


Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Msigwa amesema Rais Magufuli alitangaza siku 4 za maombolezo na sio siku za Mapumziko.

Msigwa ameandika;"Napenda kutoa ufafanuzi kuwa Jumatatu tarehe 24 Septemba, 2018 ambayo ni siku ya mwisho ya maombolezo ya Kitaifa, itakuwa ni siku ya kazi kama kawaida. Mhe. Rais Magufuli ametangaza siku 4 za MAOMBOLEZO na sio MAPUMZIKO."

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527