MBARONI KWA KUWEKA SINDANO KWENYE MATUNDA


Mtoto mmoja wa kiume nchini Australia anashikiliwa na polisi nchini humo kwa tuhuma za kuweka kwa makusudi sindano kwenye matunda aina ya stroberi (strawberry) yaliyokuwa yanauzwa katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.

Bado jeshi la polisi linafanya mahojiano na uchunguzi zaidi ili kujua ni nini hasa ilikuwa dhamira ya kijana huyo ambaye amekiri kuhusika na kitendo hicho.

Mamlaka nchini Australia zimepokea malalamiko zaidi ya 100 mapaka sasa kuhusiana na kukutwa kwa sindano katika matunda na hasa strawberry huku wakulima wa matunda hao wakituhumu matukio hayo na kudai kuna uwezekano wa kutokea kwa hasara ya zaidi ya dola milioni 160 za Kimarekani baada ya kulazimika kuyaondoa matunda hayo sokoni na kuyaharibu baada ya kuibuka kwa vitendo hivyo.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.