SHIRIKA LA WATER MISSION INTERNATIONAL LAFANIKISHA MRADI WA SAFI NA SALAMA KATA YA ZEZE WILAYANI KASULU


Afisa Tawala wa Wilaya ya Kasulu,Bw.Titus Mguha, mweye shati la kitenge akishirikiana na Meneja wa Miradi ya Maji kutoka taasisi ya Poul Due Jensen Foundation,Bw.Nils Thorup kukata utepe kuzindua mradi wa maji safi na salama katika kata ya Zeze wilayani Kasulu ambao umetekelezwa na Water Mission Tanzania, kwa udhamini wa taasisi ya Poul Due Jensen Foundation.
Afisa Tawala wa Wilaya ya Kasulu, Bw.Titus Mguha (wa pili kutoka kulia) akifuatilia matukio wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji wa kata ya Zeze ambao umejengwa na taasisi ya Water Mission Tanzania,kwa udhamini wa taasisi ya, Poul Due Jensen Foundation,wengine pichani ni Mkurugenzi wa Water Mission Tanzania Benjamin Filskov (wa kwanza kushoto),Mkurugenzi wa water Mission wa kanda ,Will Furlong (katikati) na Meneja wa Miradi ya Maji kutoka taasisi ya Poul Due Jensen Foundation,Bw.Nils Thorup
Baadhi ya wakazi wa Zeze wakicheza ngoma kufurahia kupata maji.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria katika hafla hiyo ya uzinduzi wakifuatilia matukio

Wakazi wa Kata ya Zeze iliyopo wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, kuanzia sasa wana uhakika wa kupata maji safi na salama kutokana na kuzinduliwa kwa mradi mpya wa kusambaza maji katika eneo lao.Mradi huo wenye uwezo wa kuhudumia watu karibu 5,100,umefanikishwa na Shirika lisilo la Kiserikali la kimataifa la Water Missions International Tanzania.

Serikali ya Tanzania,Water Missions International Tanzania na Poul Due Jensen Foundation ,kwa pamoja tunatambua kuwepo mahitaji ya maji safi na salama katika kanda hii na tunashirikiana pamoja na jamii zinazoishi maeneo ya miradi tumehakikisha tunaanzisha miradi endelevu ya maji safi na salama ambayo imeleta suluhisho la tatizo hili kwenye nchi za Afrika Mashariki.”

Alisema “Tunayo furaha kusheherekea uzinduzi wa mradi wa maji wa kata ya Zeze,ikiwa ni kuienzi,siku ya Niels Due Jensen,kutimiza miaka 75 ya kuzaliwa na miaka 50 ya kutoa mchango wake wa kuhudumia miradi ya kijamii kupitia taasisi ya Poul Due Jensen Foundation na kampuni ya Grundfos,”

Mwakilishi kutoka taasisi ya Poul Due Jensen Foundation,ambaye ni Meneja wa miradi ya maji,Bw. Nils Thorup alisema “Niels Due Jensen, mwenyewe ndiye alitoa maagizo kuwa pesa za msaada kutoka taasisi yake zisaidie kufanikisha miradi ya maji karibu na moja ya eneo lililopo karibu kambi za wakimbizi nchini Tanzania”.Niels siku zote anasema kufanya kazi peke yako mafanikio yake yana mipaka ila kushirikiana na watu wengi kunaweza kufanikisha kila jambo.

Ni wakati wenu wakazi wa jamii ya Zeze kushirikiana kwa pamoja kuhakikisha mradi huu tunaosheherekea kuzinduliwa kwake siku hii ya leo unakuwa endelevu.Hakuna anayeweza kufanikisha hilo peke yake bali unahitajika ushirikiano na mkifanikisha hilo mradi huu utanufaisha Watoto wenu,wajukuu mpaka vizazi vya mbele vijavyo”.

Mkurugenzi wa Water Mission Tanzania nchini,Bw.Benjamin Filskov, alieleza jinsi taasisi hiyo ilivyofanikisha miradi mbalimbali ya maji nchini Tanzania “Niels Due Jensen amekuwa mfano wa kuigwa kwangu kwa kuwa ameniwezesha kuielewa vizuri miradi endelevu ya maji na jinsi ya kuifanikisha.Ninayo furaha kuienzi dhamira yake hiyo kupitia mradi huu.”

Wakazi wa kata ya Zeze idadi yao inakaribia watu 5,100,ikiwemo watu wengine zaidi 410 ambao wanakuja kwenye taasisi za kihuduma zilizopo kwenye kata hiyo (Shule na Zahanati) ambao wanafanya idadi ya watu kufikia 5,510.Kata ya Zeze inazo shule za msingi 2,shule ya sekondari moja,zahati ndogo na makanisa.Wakazi wa Zeze wamekuwa wakipata maji kwenye visima na wengi wao wamekuwa wakitayumia kwa kunywa bila kuyaweka katika mazingira ya usafi zaidi.

Kwa upande wake,Afisa Tawala wa Wilaya ya Kasulu,Titus Mguha ,amesema mradi huu ni wa kihistoria kutokana na eneo hilo kuwa na changamoto ya maji kwa muda nrefu “Kwa niaba ya Serikali napenda kuzishukuru taasisi za Water Mission Tanzania, the Niels Due Jensen Foundation na Grundfos kwa jitihada zao ambazo zimefanikisha wakazi wa eneo hili wanapata maji safi na salama”alisema.

Alisema,kabla ya kuanzishwa mradi huu,wanawake walikuwa wakisafiri umbali mrefu kutafuta maji na maji waliyokuwa wakiyapata hayakuwa salama ambapo yalisababisha kuwepo kwa milipuko mbalimbali ya magonjwa kwenye jamii hiyo.

Alitoa wito kwa wanufaika wa mradi huo kuwa sehemu ya mradi huo na siku zote kuwa mstari wa mbele kulinda miundombinu ya mradi na kuwapa ushirikiano wataalamu wanaosaidia kuufanikisha “Kama Serikali ya wilaya tuko tayari kushirikiana na Water Mission Tanzania,kuhakikisha mradi huu unakuwa endelevu katika eneo hili ambalo linakua kwa kasi,”alisema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527