SERIKALI MKOA WAKATAVI WAANZA KUSIMAMIA GHARAMA ZA MBOLEA KWA WAKULIMA

Uongozi  wa   mkoa wa Katavi  umesema  utahakikisha  changamoto  za  ucheleweshaji wa mbolea za kupandia  na  kukuzia kwa msimu wa kilimo wa mwaka 2018-2019  zinaisha  kwa kuwasimamia  mawakala    kutoka  kampuni   ya Yara kupitia kwa wakala wake mkuu Obo investment ili  kufanikisha kupatikana kwa mbolea mapema kabla ya msimu wa kilimo haujaanza na kuleta usumbufu kwa wakulima wa mkoa huo.

Hayo yamezungumzwa  na Kaimu katibu tawala mkoa wa Katavi CRESENCIA JOSEPH  mara  baada ya kuzindua ghala kubwa la kuhifadhia  mbolea na kufungua mafunzo  elekezi ya matumizi sahihi ya mbolea kwa wakulima na maafisa kilimo wa kata na vijiji katika mkoa wa katavi

Akizungumza   katika mafunzo ya matumizi sahihi ya pembejeo za kilimo kwa maafisa kilimo na wasambazaji wa pembejeo,Mkurugenzi wa Kampuni ya Obo investment Olais  Oleseenga amesema wameamua kuweka Ghala kubwa mkoani katavi ili kuhakikisha wakulima wa mkoa huo na mikoa jirani wanapata pembejeo kwa haraka kupitia wauzaji wadogo na wakubwa.


Olais amesema OBO Investment ikiwa wakala mkuu wa kampuni ya Mbolea ya YARA watahakikisha mbolea inapatikana katika katika kipindi chote na siyo kama ilivyo sasa katika maeneo mengi ambapo mbolea inaanza kupelekwa wakati wa msimu hali inayosababisha kuchelewa kutokana na ubovu wa miundo mbinu pamoja na umbali wa walipo wahitaji na watahakikisha bei za mbolea zitakua ndogo kwa mkulima mala baada ya kuanza kutumia usafiri treni kutoa mbolea kutoka Dar es salaam mpaka Mpanda katavi

Ameongeza kuwa katika mkoa wa Katavi wanatarajia kuwa na wauzaji wa pembejeo wapatao 100 katika wilaya 3 ambao watapewa mafunzo ya matumizi bora ya pembejeo itakayowasaidia kuwapa elimu wakulima wa mazao mbali mbali mkoani humo wakiwemo wa Mpunga,Mahindi,Mboga mboga na mazao mengine.

Naye Afisa Biashara wa kampuni ya YARA nyanda za juu kusini John Meshak amesema wameamua kuzindua ghala la mbolea Mpanda kwa kuwa kuna wakulima wengi wanaolima mazao mengi ila hawapati nafasi ya kupata mbolea bora na kwa wakati hali inayopunguza kasi ya uzalishaji wa mazao yao.

Kwa niaba ya wakulima wa mkoa wa katavi akiongea kwa niaba ya wakulima wenzake ameipongeza kampuni ya OBO Investment ambao ni wakala mkuu wa YARA kwa kuwafikishia pembeo kwa wakati,na kuongeza kuwa kuanzia msimu ujao uzalishaji utaongezeka kwa kuwa wakulima wamelima na kuwekea mbolea kwa wakati tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Mwishoni mwa mwaka jana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alitoa wito kuhakikisha kwamba Mbolea na pembejeo zingine zinapatikana muda wote zinapohitajika tena na kwa gharama nafuu ambapo Kampuni ya OBO Investment ambao ni wakala wakuu wa Kampuni ya Mbolea ya YARA wameanza kutekeleza agizo hilo kwa mikoa ya Mbeya,Songwe, Rukwa, na Katavi.









Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527