RC KAGERA AAGIZA JESHI LA POLISI,TAKUKURU KUSIMAMIA KCU 1990 LTD NA KDCU LTD KURUDISHA MIL 483


Mkuu wa mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco  Gaguti  akitoa maagizo kwa viongozi wa Vyama vya ushirika Kagera.

Na Angela Sebastian - Malunde1 blog

Mkuu wa mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco  Gaguti aagiza Jeshi la Polisi na Kamanda wa TAKUKURU Mkoani Kagera kuvisimamia Vyama Vikuu vya Ushirika vya KCU 1990 Limited na KDCU Limited kurejesha fedha za wakulima Shilingi Milioni 483 ambazo zimetumika kinyume na utaratibu uliopangwa.


Mkuu wa Mkoa Gaguti ametoa agizo hilo leo Septemba 6, 2018 ofisini kwake mara baada ya kupata taarifa kuwa Vyama hivyo Vikuu viwili vilikopa fedha hizo kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania kwa ajili ya kuwalipa wakulima kutoka kwenye Vyama vya Msingi lakini Vyama hivyo Vikuu vimezitumia fedha hizo kinyume na malengo.

“Nimepata taarifa kuwa Vyama hivi viwili vimetumia shilingi milioni 483 kwa kujilipa mishahara na kuwalipa wazabuni wakati fedha hizo zilikopwa kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania kwaajili ya kuwalipa Wakulima kutoka Vyama vya Msingi, uongozi wa Mkoa haukubaliani na suala hili”,lifafanua Gaguti.

Aidha, Gaguti alimuagiza Kamanda wa Polisi mkoa na Kamanda wa TAKUKURU Mkoa kuanzia saa 2:00 asubuhi kuvisimamia Vyama Vikuu hivyo viwili kufanya kazi chini yao kwa masaa 24 na taarifa kutolewa fedha zilitumika vipi aidha, fedha hizo ziwe zimerejeshwa ndani ya siku saba.

Chama Kikuu cha KCU 1990 Limited kimetumia Shilingi Milioni 206 na KDCU Limited kimetumia Shilingi Milioni 282.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527