RAIS MAGUFULI ATEUA MKURUGENZI MPYA WA TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA (TAKUKURU)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Kamishna wa Polisi Diwani Athumani kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).


Uteuzi wa Kamishna Diwani Athumani unaanza leo tarehe 06 Septemba, 2018. Kabla ya uteuzi huo Kamishna Diwani Athumani alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera.


Kamishna Diwani Athumani anachukua nafasi ya Kamishna wa Polisi Valentino Mlowola ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527