Wednesday, September 12, 2018

RAIS ACHEZA DAKIKA 79 MECHI YA KIRAFIKI

  Malunde       Wednesday, September 12, 2018
Rais wa Liberia George Weah alicheza mechi ya kirafiki ya kimataifa kwa nchi yake siku ya Jumanne akiwa na miaka 51.

Weah ambaye ni mchezaji wa kwanza wa soka kutoka Afrika kushinda tuzo la mchezaji bora wa Fifa, alicheza dakika 79 kwenye mechi ambapo walishindwa na Nigeria kwa mabao 2-1 nyumbani Monrovia.

Liberia ilipanga mechi hiyo ya kirafiki kupumzisha shati namba 14 ambalo lilitumiwa na Weah wakati wa kilele cha taaluma yake.George Weah alichezea Monaco, Paris St-Germain na AC Milan - akikaa muda mfupi Chelsea na Manchester City

Mchezaji huyo wa zamani wa AC Milan, ambaye aliapishwa kuwa Rais mwezi Januari, alishangiliwa wakati akitolewa uwanjani wakati wa mabadiliko.

Nigeria ilikuwa na kikosi kikali akiwemo Wilfred Ndidi wa Leicester na mwenzake Peter Etebo wa Stoke City.

Etebo alipiga kona ambayo Simeon Nwankwo aliitumia kuiweka Nigeria kifua mbele kwa mabao 2-0 baada ya Henry Onyekuru ambaye yuko kwa mkopo huko Galatasaray kutoka Everton kufunga bao la kwanza. Liberia walifunga bao lao kwa njia ya penalti iliyopigwa na Kpah Sherman.
Chanzo - BBC
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post