RAIS MAGUFULI ATUMBUA WAWILI NA KUTEUA WENGINE


Rais Dkt. John Magufuli leo Septemba 03, 2018 amemteua Dkt. John Antony Kiang’u Jingu kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto).

Kabla ya uteuzi huu Dkt. Jingu alikuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Dkt. Jingu anachukua nafasi ya Bi. Sihaba Nkinga ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Gabriel Pascal Malata kuwa Kamishna wa Kazi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.

Kabla ya uteuzi huo Bw. Malata alikuwa Mkurugenzi Msaidizi Kesi za Madai, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Bw. Malata anachukua nafasi ya Bi. Hilda Nkanda Kabisa ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post