RAIS MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA POLE KWA WAANDISHI WA HABARI WALIOPATA AJALI


Rais Dk. John Magufuli ametuma salamu za pole kwa Waandishi wa Habari na watu wengine waliopata ajali katika Msafara wake wa Ziara ya fupi mkoani Mwanza.

Akifikisha salamu hizo za pole, kwa Wanahabari Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amesema kuwa Rais ametambua mchango wa Waandishi wa Habari toka alipofika jijini hapa 3, Septemba 2018 na kuzindua miradi mbalimbali ikiwemo utiaji saini mkataba wa Kandarasi ya ujenzi wa meli kubwa ya kisasa.

"Waandishi wa Habari wamefanya kazi kubwa mimi mwaka wa tatu nipo jijini hapa mnatueleza changamoto ziko wapi naomba tuendelee hivyo kuchangia maendeleo ya nchi yetu," alisema Mongella.

Akizungumzia ajali hiyo iliyotokea kwenye msafara wa Ziara ya fupi ya Rais iliyotokea wilayani bunda kuelekea kisorya ilisababishwa na vumbi kuwa jingi na kupelekea mtikisiko katika gari la Waandishi wa Habari ambapo baadhi yao walipata majeraha.

Aidha mmoja kati ya Wanahabari waliopata ajali hiyo Emmanuel Meshack aliyeumia sehemu ya bega na goti la mguu, ameshukuru Serikali ya Mkoa kutambua umuhimu wao na kuomba wasisite kutoa ushirikiano kwa waandishi kwa maendeleo ya Taifa.

Na James Timber, Mwanza

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post