PROF. MKUMBO AWASHAURI WAHANDISI KUWA NA MAJIBU KABLA YA WANASIASA KUWAULIZA MASWALI KUHUSU MIRADI


Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo. 

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo amewashauri wahandisi nchini kujenga utamaduni wa kuandaa mipango ya miradi ya maendeleo ya maji na kuwa na majibu kabla ya kukutana na maswali ya viongozi wa kisiasa.

Profesa Kitila ametoa ushauri huo leo wakati akiwasilisha mada yake inayohusu maendeleo ya maji kwa wahandisi ambao wapo katika maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa Bodi ya Usajili Wahandisi wa Tanzania (ERB) yanayofanyika jijini Dar es Salaam.

Hivyo wakati anatoa mada hiyo pamoja na mambo mengine amewaambia iwapo watakuwa na mipango inayoonesha gharama za miradi mbalimbali inayotekelezwa itakuwa rahisi kujibu maswali ya viongozi wa kisiasa bila kuchelewa badala ya kusubiri kuulizwa.

"Wahandisi wengi wamekuwa wakisubiri maelekezo kutoka kwa wanasiasa hali ambayo inachelewesha maendeleo ya miradi ya maji hasa vijijini.Ni vema wahandisi wakawa mbele kwa.majibu na hiyo itawezekana kwa kuwa na mipango endelevu," amesema.

Ameongeza kuwa "Wahandisi wanatakiwa kuwa mbele ya wanasiasa kwa kuwa mipango ya maendeleo na hasa miradi ya maji ili kuepuka maelekezo ambayo sio ya kitaalamu," amesisiza na kueleza maji na maendeleo na maendeleo na maji.

Prof.Kitila amewasisitiza wahandisi nchini kiwa ili miradi ya maji kuwa na tija wana kila sababu ya kuwa wabunifu kwa kubuni miradi mipya na kubwa ni kutatua changamoto zilizopo.

"Ni wajibu wa wahandisi kuhakikisha wanabuni miradi ya maji,kwa mfano wanaweza kubuni mradi wa maji wa kuondoa changamoto Singida kwa kutumia maji yaliyopo Ziwa Victoria," amesema.

Amefafanua kwa kufanya hivyo hata akitokea kiongozi akazungumzia utatuzi wa maji mkoani Singida tayari wahandisi walishakuwa na majibu na kinachobaki ni utekelezaji.

Kuhusu mikakati ya Serikali katika sekta ya maji nchini, Profesa Mkumbo amesema kuna mpango wa miaka mitano ambao utagharimu zaidi ya Sh.Tril 10.4 kwa lengo la kufanikisha upatikanaji wa maji.

Akizungumzia kiasi cha maji kilichopo nchini Profesa Mkumbo Kuhusu kiasi cha maji kilichopo Kitila alisema hali bado ni nzuri ambapo pamoja maji kupungua Tanzania ina ujazo wa trilioni 92.

Pia ametoa mwito kwa kila mwananchi kuendelea kutunza vyanzo vya maji ili kunufaisha vizazi vya sasa na vijavyo huku akiwasisitiza wahandisi kutambua dhamana walinayo katika maendeleo ya nchi.

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527