RAIS MAGUFULI APOKEA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA KUFUA UMEME WA STIEGLER"S GORGE IKULU DAR


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi waandamizi wa serikali wanaosimamia utekelezaji wa mradi wa kufua umeme katika Mto Rufiji wa Stiegler's Gorge wakisimama kwa dakika kadhaa kuwakumbuka marehemu waliopoteza masiha kwenye ajali ya kivuko cha MV Nyerere huko Ukara wilayani Ukerewe mkoa wa Mwanza majuzi. Hii ilikuwa ni kabla ya kuanza kwa kikao kazi ambapo alipokea taarifa ya maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 24, 2018.Picha na Ikulu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na viongozi waandamizi wa serikali wanaosimamia utekelezaji wa mradi wa kufua umeme katika Mto Rufiji wa Stiegler's Gorge pamoja na wataalamu wakati wa kikao kazi ambapo alipokea taarifa ya maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 24, 2018.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527