Picha : TCRA YAENDESHA WARSHA KUHUSU RASIMU YA MKATABA KWA WATEJA KWA WADAU SHINYANGA



Mamlaka ya mawasiliano nchini Tanzania TCRA, imeendesha warsha ya siku moja kwa wadau wa sekta ya mawasiliano mkoani Shinyanga, kwa lengo la kutoa maoni ya rasmu ya mkataba kwa wateja wa mamlaka hiyo ili kuufanyia marekebisho kabla ya kuchapishwa na kuanza kufanya kazi rasmi.


TCRA imeendesha warsha hiyo leo Septemba 25,2018 katika ukumbi wa mikutano wa Empire Hotel mjini Shinyanga, kwa kukutananisha wadau wa sekta hiyo ya mawasiliano kutoka makampuni yaliyo na leseni za mamlaka hiyo ambao ni Bloggers, Radio, Cables pamoja na Simu za mkononi.

Akisoma hotuba ya ufunguzi wa warsha hiyo kwa niaba ya mkurugenzi mkuu wa TCRA kutoka makao makuu jijini Dar es salaam Eng James Kilaba, Mhandisi mkuu wa TCRA kutoka Kanda ya ziwa  Eng. Lawi Odiero, amesema mikataba hiyo ya huduma kwa wateja itatumika kama chombo cha kuzuia rushwa katika utoaji wa huduma kwa wateja wa mamlaka hiyo.

Amesema hivi karibuni kumekuwa na mikataba ya huduma kwa wateja inatolewa kwa wingi, lengo likiwa ni nyenzo ya kuzirekebisha taasisi za Serikali ili ziweze kumjali mteja, na kutekeleza majukumu yake kwa uwazi na kwa kuzingatia dhana ya uwajibikaji na utawala bora.

“Mtakumbuka kwamba TCRA, Mnamo Julai 16,2018 tulifanya uzinduzi wa rasmi ya mkataba kwa mteja wetu pamoja na kuzindua kampeni ya kupambana na rushwa, ili kuongeza utendaji kazi wa mamlaka yetu, na mdau wa mawasiliano endapo ukiombwa rushwa atupe taarifa mapema ilitupate kumshughulikia mhusika,”amesema Eng. Odiero.

Aidha amesema Mkataba huo kwa wateja utakuwa ni kinga muhimu ya kuzuia malalamiko kwa watendaji kazi wa TCRA katika kuboresha huduma pamoja na kuziba mianya ya rushwa kwenye ofisi za mamlaka hiyo.

Naye Mhandisi wa mamlaka hiyo Imelda Salum, amesema Mkataba huo pia utasaidia kulinda maslahi ya wadau hao wa mawasiliano, pamoja na kukuza uelewa juu ya kuzitambua haki zao ikiwamo na kuwapatia huduma haraka kwa kuzingatia sheria.

Nao baadhi ya wadau hao wa mawasiliano ,waliipongeza TCRA kwa kukutana nao, na kutumia fursa hiyo kuwasilisha kilio chao hasa kwa upande wa Ving’amuzi, kuwa pindi vifurushi vinapoisha channel za nyumbani hazionyeshi kinyume na utaratibu, na kupewa majibu kuwa suala hilo kwa sasa linashughulikwa.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI


Mhandisi mkuu wa TCRA Kanda ya ziwa Lawi Odiero akisoma hotuba ya ufunguzi ya warsha ya wadau wa sekta ya mawasiliano mkoani Shinyanga, na kuwaeleza madhumuni ya kuwasilisha maoni juu ya kurekebisha rasmu ya mkataba kwa wateja wa mamlaka hiyo kabla ya kuchapishwa rasmi ambao utakuwa mkombozi kwao katika kuwa boreshea huduma na kuzuia mianya ya Rushwa.- Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog

Mhandisi wa mamlaka TCRA Imelda Salum,akizungumza kwenye warsha hiyo ambapo amesema Mkataba huo pia utasaidia kulinda maslahi ya wadau hao wa mawasiliano, pamoja na kukuza uelewa juu ya kuzitambua haki zao ikiwamo na kuwapatia huduma haraka kwa kuzingatia sheria.

Ofisa kutoka taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Takukuru mkoani Shinyanga Alice Mazoko akielezea madhara ya kuomba na kutoa rushwa katika warsha hiyo ya wadau wa mawasiliano ambao ni wateja wa TCRA.

Wakili kutoka taasisi ya kupambana na Rushwa mkoani Shinyanga Takukuru Wilfred Komba akielezea makosa ya rushwa hadi kutungwa kwa sheria za kupambana na rushwa mwaka 2007 kutoka makosa nane hadi 24.

Wadau wa mawasiliano mkoani Shinyanga wakiendelea na warsha kutoka TCRA inayohusu mashauriano ya Rasimu ya mkataba kwa wateja,( TCRA CLIENT SERVICE CHARTER).

Warsha ikiendelea katika ukumbi wa mikutano katika hoteli ya Empire mjini Shinyanga.

Warsha ikiendelea katika ukumbi wa mikutano katika hoteli ya Empire mjini Shinyanga.
Warsha ikiendelea katika ukumbi wa mikutano katika hoteli ya Empire mjini Shinyanga.

Warsha ikiendelea 

Wadau wakiwa ukumbini



Warsha inaendelea 

Warsha ikiendelea katika ukumbi wa mikutano katika hoteli ya Empire mjini Shinyanga.

Saidi Juma kutoka Walda Cable Network mjini Shinyanga akiuliza swali kwenye warsha hiyo.

Simeo Makoba ambaye ni Programu meneja kutoka Radio Faraja akiuliza swali kwenye warsha hiyo 

Warsha inaendelea

Silvester Rwekiza kutoka kampuni ya Simu Tanzania TTCL akiuliza swali kwenye warsha hiyo.

Haji Ngalama alimaarufu kwa jina la kisanii (Nura) akiwakilisha Ngalama Cable kutoka mjini Shinyanga akiuliza swali kwenye warsha hiyo.

Awali kabla ya kuanza kwa warsha hiyo ,Viongozi wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA wakiwa wamesimama kwa dakika moja kuwaombea watu wote waliofariki kwenye ajali ya kivuko cha MV Nyerere Septemba 20,2018.

Wadau wa sekta ya mawasiliano mkoani Shinyanga wakiwa wamesimama kwa dakika moja kuwaombea watu waliofariki kwenye ajali ya kivuko cha MV Nyerere

Wadau wa sekta ya mawasiliano mkoani Shinyanga wakiwa wamesimama kwa dakika moja kuwaombea watu waliofariki kwenye ajali ya kivuko cha MV Nyerere

Picha zote na Marco Maduhu- Malunde1 Blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post