HALMASHAURI YA WILAYA GEITA YATUMIA MAONESHO YA DHAHABU KUTANGAZA WAJASIRIAMALI


Halmashauri ya Wilaya ya Geita imetumia Maonyesho ya Dhahabu kutangaza bidhaa mbalimbali zinazo zalishwa na vikundi 55 vya wajasiriamali ambao wananufaika na fedha za mikopo ya 10% kutoka katika Halmshauri hiyo katika makundi ya wanawake ,vijana na walemavu.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo,Afisa Habari wa Halmashauri hiyo Godfrey Nsajigwa akiwa  katika kiwanja cha Kalangalala Geita mjini katika mabanda ya maonesho ya bidhaa hizo amesema vikundi hivyo vinanufaika na mikopo ambayo ni pesa za Halmashauri hiyo zinazo kusanywa kutokana na mapato ya Dhahabu.

Ameeleza kuwa Halmashauri hiyo inatoa mikopo 10% ya mapato yake ya ndani kwenda kwa makundi ya vijana,wanawake na walemavu ambapo kundi la wanawake wanakopeshwa 4% ,vijana 4% na walemavu 2% kwa sasa wana vikundi zaidi ya 50 vikiwemo vikundi viwili vya walemavu ambao katika maonyesho hayo wanauza viatu.

Nsajigwa amesisitiza kuwa,Halmashauri imeamua kutumia maonesho hayo kusaidia wajasiriamali hao kutangaza bidhaa zao kama njia njia ya kupata masoko kwa bidhaa hizo ili waendelee kunufaika kwa kuuza bidhaa zao kupitia maonyesho ya Dhahabu.

Maonyesho hayo yameanza tarehe 24 Septemba mwaka huu na yatazinduliwa rasmi na Waziri wa Madini Angella Kairuki tarehe 26 Septemba na washiriki wapatao 250 wenye mabanda ya maonesho wakitarajiwa kushiriki na yatahitimishwa tarehe 30 Septemba mwaka huu.

Na Mutta Robert - Geita.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527