MKUU WA MKOA ATAKA WALIMU WANAOPIGA WANAFUNZI WACHAPWE BAKORA

Katika kuhakikisha kitendo kilichotokea mkoani Kagera cha mwanafunzi kupigwa na kusababishiwa kifo hakitokei mkoani Tanga, mkuu wa mkoa huo Martine Shigela amewaagiza viongozi wa mkoa huo kusimamia sheria za adhabu mashuleni.


Akiongea jana kwenye kikao cha robo ya tatu ya mwaka cha kamati ya ushauri ya mkoa (RCC), Mh. Shigela alisema mwalimu atakayebainika kutoa adhabu kinyume na utaratibu naye aweze kuadhibiwa kama ilivyokuwa kwa mwanafunzi.


''Mwalimu akienda kinyume na sheria ya adhabu mashuleni maana yake kajitengenezea sheria yake ambayo haijatungwa na bunge hivyo kwa kosa hilo lazima iwepo adhabu kwa mwalimu aliyevunja sheria na kwasababu anakuwa ametoa adhabu ya viboko ni vyema na yeye akapata viboko kama alivyo mchapa mwanafunzi'', alisema.


Kwa upande wake afisa elimu mkoa wa Tanga Mayasa Hashim amewaasa walimu kufuata utaratibu wa aina ya adhabu anazopaswa kupewa mwanafunzi huku akiongeza kuwa sio kila kosa linahitaji adhabu bali makosa mengine yanatakiwa kuishiwa kwa mwalimu kumshauri mtoto ili asirudie.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527