MIZIGO YA WALIOFARIKI,MANUSURA KWENYE KIVUKO CHA MV NYERERE YAANZA KUELEA ZIWANI

Baadhi ya mizigo ikiwamo mikungu ya ndizi, mikoba na majamvi iliyokuwa ndani ya kivuko cha Mv Nyerere kilichozana ziwa Victoria imeanza kuelea na kusukumwa na maji hadi ufukwe wa kijiji cha Bwisya kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe mkoani Mwanza.

Hali hiyo imejitokeza baada ya wataalam wa uokoaji kufanikiwa kikilaza ubavu kivuko hicho hicho kilichopinduka Septemba 20 na kujifunika kifudifudi.

Na Peter Saramba, mwananchi
    Theme images by rion819. Powered by Blogger.