LUGOLA ATOA UFAFANUZI MAHABUSU KUKAA MASAA 24 POLISI BILA KJUFIKISHWA MAHAKAMANI

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema suala la mtuhumiwa kukaa mahabusu saa 24 linazingatia suala la upelelezi wa awali hivyo mtu akitolewa humo kusaidia kupeleleza muda huanza kuhesabiwa upya anaporudishwa ndani.


Amesema, kwenye Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai mtuhumiwa anapokamatwa kwa mara ya kwanza na kuwekwa mahabusu anaweza kutolewa kabla ya kufika saa 24 kwa ajili ya upelelezi au kwenda kuonesha silaha au kuonesha ushahidi kutokana na maelezo yake.


"Mnapomtoa atakaporudi mahabusu huyo mtuhumiwa anaanza kuhesabiwa masaa yake upya. Sasa kwa bahati mbaya wananchi wanahesabu tangu tangu alipokamatwa lakini kisheria tunahesabu tofauti"alisema jana Waziri Lugola wakati anajibu swali la Mbunge wa Tarime Vijijini John Heche.


Heche alitaka Waziri Lugola atoe tamko kwamba polisi wazingatie sheria na iwezo marufuku kwa mtuhumiwa kuwekwa mahabusu zaidi ya saa 24 bila kufikishwa mahakamani.


Lugola alisema, si nia ya Serikali kutesa wananchi hivyo askari watakaokiuka sheria hiyo ya mahabusu saa 24 watachukuliwa hatua.


"Hakuna yeyote ambaye sisi tunamfumbia macho. Kwa hiyo Mheshimiwa Heche uwe na amani. Huyo mtu unayemsema huyo tumeshatoa maelekezo, na tunajua concern yako"alisema Lugola.


Alikiri kuwepo kwa malalamiko ya wananchi kuwekwa nani na baadhi ya polisi wasio waaminifu na waadilifu kwa makosa yasiyostahili.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post