MWILI WA MTOTO WAOPOLEWA ZIWA VICTORIA AJALI YA MV NYERERE...IDADI YA VIFO YAFIKIA 225

Mwili mmoja wa mtoto umepatikana saa nne asubuhi hii, wakati wazamiaji wakiweka sehemu ya chini Maputo (boya) yanayojazwa upepo ili kukiinua kivuko cha MV Nyerere, eneo la Bwisya kisiwani Ukara, jijini Mwanza.

Kazi ya kukinyanyua kivuko hicho kilichozama Alhamisi iliyopita na kusababisha vifo vya watu 225 ilianza jana Jumamosi Septemba 23,2018.
Kazi hiyo inafanywa na kampuni ya Songoro Marine chini ya usimamizi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Akizungumza mbele ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika Kijiji cha Bwisya Kisiwa cha Ukara kilipozama kivuko hicho, mtaalamu kutoka kampuni hiyo, Meja Songoro alisema hatua ya kwanza itakuwa kuingiza hewa ndani ya kivuko ili kuyatawanya maji na kuanza kukivuta.

“Kivuko kinaendelea kuelea kwa sababu kuna hewa ndani yake. Wakati kinageuka (kupinduka) kilichota maji, tutaanza kuingiza hewa kutoa maji na kuanza kukivuta. Tutakapoanza kuyatawanya maji hayo, pia tutapeleka boya na hii itafanya chombo kizidi kuja juu. Baada ya hapo tutakisogeza taratibu hadi kwenye maji mafupi.”

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527