Breaking : MFALME WA REGGAE TANZANIA JAH KIMBUTE AFARIKI DUNIA USIKU HUUNa Sultani Kipingo wa Globu ya Jamii

Habari zilizotufikia usiku huu zinasema kwamba gwiji wa muziki wa reggae nchini Jah Kimbute amefariki dunia nyumbani kwake Msasani jijini Dar es salaam, mshirika wa karibu wa marehemu David Msitta Manju, amethibitisha.

Akiongea nasi kwa njia ya simu kutoka Mwanza aliko kikazi, Manju amesema amepata habari usiku huu kwamba Jah Kimbute amefariki dunia Alhamisi jioni nyumbani kwake.

Amesema kwamba amepata taarifa hizo toka kwa mkewe aliyeko jijini Tanga na kwamba mipango ya mazishi itajulikana leo asubuhi baada ya ndugu kukusanyika.

Mke wa marehemu pia alithibitisha habari hizo akiwa Tanga, na kusema kila kitu kitafahamika baada ya ndugu wa Jah Kimbute kukutana.

Amesema marehemu alikuwa akiishi na mwanae nyumbani kwake Msasani na kwamba jana jioni alipokwenda chumbani kwake alimkuta amefariki.

"Hizi habari tumezipata usiku huu na sasa ndugu wa marehemu ambao wengi wako Lushoto wanakusanyika tayari kwa safari ya Dar es salaam kesho kukamimlisha mipango yote.

Jah Kimbute, ambaye jina lake halisi alikuwa Samwel Mleteni, alitamba sana katika anga ya muziki na kuitwa Mfalme wa Reggae wa Tanzania miaka ya 80 akiwa na kundi lake la Roots and Culture lililokuwa na makaazi yake jijini Dar es salaam.

Chanzo- Michuzi blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post