KIVUKO CHA MV NYERERE CHAZAMA ZIWA VICTORIA...MAMIA WAHOFIWA KUFA

Mamia ya watu wanahofiwa kufariki baada ya kivuko cha MV Nyerere walichokuwa wanasafiria kuzama katika ziwa Viktoria mkoani Mwanza magharibi mwa Tanzania.

Wizara ya uchukuzi na mawasiliano Tanzania TEMESA imetoa taarifa ikithibitisha mkasa huo kilichotokea kati ya Ukara na Bugolora wilayani Ukerewe majira ya mchana.

Maafisa wa serikali nchini wamethibitisha kwamba shughuli ya kuwaokoa manusura inaendelea.

Taarifa za awali zinaeleza kwamba kivukio hicho kilikuwa kimebeba mamia ya abiria.

Kamishna wa eneo jirani la Mara, Adam Malima ameeleza kwamba maafisa kadhaa kutoka enoe hilo wakiwemo polisi na jehsi la majini wanaelekea kujiung akatika jitihada za uokozi.

''Hatuijui hali halisi tunakwenda kuikagua kwanza alafu baadaye tutatoa tamko rasmi.

Malima ameeleza kwamba maboti ya polisi na jeshi watashirikaian akatika zoezi hilo la uokozi.

''Tunaomba mungu atupe subira kwa wakati huu, na tusishuhudie idadi kubwa ya vifo

Mkasa huo umewashutusha wengi nchini kama mwanamke mmoja aliyeshuhudia mkasa huo ambaye alionekana kujawa na hisia.

''Tazama Tazama.. Kivuko kile pale kimezama …….miili inaelea, imezama sasa hivi''.Umati mkubwa wa watu umeshuka ufukweni kutazama jitihada za uokozi

Mikasa ya vivukio kuzama Tanzania

Tanzania ina historia ya ajali za vivukio kuzama, kibaya zaidi kuwahi kushuhudiwa kilikuwa ni mnamo Mei 1996, wakati MV Bukoba kilipozama kutoka Mwanza katika ziwa lilo hilo Viktoria magharibi mwa Tanzania na kusababisha vifo vya takriban watu 1000.

Rekodi rasmi hatahivyo iliopo ni watu 894 waliofariki.

Kumewahi kushuhudiwa pia mikasa mingine kama vile Mv Skagit kivukio kilichozama mnamo 2012 wakatikikiwa kimebeba abiria 290 wakiwemo watalaii 17 kutoka pwani ya Zanzibar.

Mwanza ni mji muhimu wenye bandari Tanzania katika ziwa Viktoria, inayopokea bidhaa kama pamba chai, kahawa zinazotoka magharibi mwa nchi hiyo.

Ziwa viktoria ni la pili kwa ukubwa duniani baada ya ziwa Superior Amerika kaskazini.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post