GUNINITA KUZIKWA JUMATANO SEPTEMBA 19,2018 MOROGORO

Mwili wa Mwenyekiti wa zamani wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita unatarajiwa kuzikwa Jumatano Septemba 19, 2018 kijijini kwao Kibaoni, Ifakara mkoani Morogoro.


Guninita ambaye jina lake linabaki katika orodha ya wanasiasa wenye uwezo wa kutenda kile wanachoamini alifariki dunia jana Septemba 13, 2018 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) alikokuwa akipatiwa matibabu.


Mdogo wa marehemu, Gerald Guninita amesema mwili wa kaka yake utachukuliwa MNH Jumanne asubuhi, misa ya mazishi itakayofanyika nyumbani kwake Tabata Kimanga.


Amesema, awali Guninita alikuwa anasumbuliwa na kwiwi, kiungulia na baada ya vipimo alibainika kuwa na uvimbe tumboni.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527