GODBLESS LEMA AMNADI MGOMBEA UBUNGE CHADEMA UKONGA

Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amesema kitendo cha Asia Msangi kujitokeza kugombea ubunge Ukonga ni ujasiri ambao unatakiwa kuungwa mkono kabla hata hajasema atafanya.

Lema ameyasema hayo jana Septemba 2, 2018 kwenye kampeni za Chadema zilizofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Chanika, jijini Dar es Salaam.

Alisema wanaume wa Dar es Salaam wamekuwa ni waoga na wanarubuniwa na fedha au kuahidiwa vyeo.

Alisema yeye ataendelea kupigania haki za wanyonge licha ya vitisho vingi dhidi ya wapinzani.

Lema ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema amewataka wakazi wa Chanika kumchagua mgombea huyo ili akaungane naye kwenye harakati za kujenga demokrasia.

Alisema Chadema imeibiwa kura kwenye chaguzi za Kinondoni na Siha, hivyo amewataka siku ya uchaguzi kujitokeza kwa wingi kupiga kura na kulinda kura zao.

"Hamna dhambi kubwa kama uoga, msitishwe na hawa polisi, ninyi mna nguvu kubwa kuliko wao. Uchaguzi huu si kati ya Asia na Mwita bali ni kati ya nuru na giza," alisema Lema.

Mbunge huyo amesema vita inayoendelea ni ya demokrasia dhidi ya watu wanaotumia nguvu kubwa kuua demokrasia ya Tanzania.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527