DIWANI WA KATA YA CHAMAZI,AKABIDHI JEZI KWA TIMU YA WASICHANA YA UVCCM TAWI LA KWA MKONGO

Diwani wa kata ya Chamazi Mh. Hemedi Karata  alikabidhi jezi seti moja timu ya mpira ya wanawake ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi tawi la Kwa Mkongo (Kwa Mkongo Queens) inayo jianda na Mashindano ya Mpira wa Rede inayofamika kama MSOLOGONI REDE CUP 2018 inayotarajia kuanza kutimua vumbi Septemba 21,2018 katika Uwanja wa Kwa Karata, Chamazi, Dar es Salaam.

Akizungumza jana jioni mara baada ya kukabidhi jezi Mhe.Karata alipongeza timu hiyo na kuwaomba kudumisha umoja na ushirikiano walio kuwa nao.

"Niwapongeze sana, taarifa zenu ninazo kuwa mnafanya vizuri sana, ivyo na mimi nimeamua kuja kuwaunga mkono kwa kuwaletea seti moja ya jezi"

"Niliambiwa mnajianda na mashindano ambayo yanaanza tarehe 21 mwezi huu,na shida yenu kubwa ilikuwa jezi ndiyo maana nikaona niwalete, pia naimani kubwa na timu hii kufanya vizuri katika mashindano hayo, ivyo niwatakie kila la kheri" alisema Mhe. Karata.

Mhe.Karata alisema kuwa moja ya sehemu ya ulezi wa timu hiyo.

Imetolewa na

Shabani Rapwi

Katibu Hamasa na Chipukuzi Tawi la Kwa Mkongo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post