Sunday, September 9, 2018

BONDIA MTANZANIA AMCHAPA MUINGEREZA

  Malunde       Sunday, September 9, 2018

Bondia, Hassan Mwakinyo akifurahia ushindi

Mwanamasumbwi raia wa Tanzania, Hassan Mwakinyo amemchakaza bondia, Sam Eggington raia wa Uingereza kwa KO katika raundi ya pili mjini Birmingham nchini Uingereza.

Pambano hilo lililofanyika usiku wa jana, lilishuhudia Mwakinyo akiendeleza rekodi nzuri katika michezo yake huku akionekana kumshinda mpinzani wake tangu mwanzo wa mchezo kwenye pambano lililochukua takribani dakika 10 kupata mshindi.

Hassan Mwakinyo (23) ambaye ni bingwa wa mkanda wa WBA sasa ameshinda michezo 12 kati ya 14 aliyocheza huku akipoteza mapambano mawili pekee.

Mpinzani wake, Sam Eggington ambaye ni bingwa wa mkanda wa WBC sasa anakuwa amefikisha mapambano 28 aliyopigana, akishinda 23 na kupoteza mapambano matano ukiwemo huo wa jana dhidi ya Mwakinyo.

Kipigo hicho cha Eggington kinampunguzia nafasi nzuri ya mipango yake ya kuandaa mapambano makubwa mwaka huu.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post