BOBI WINE ARUHUSIWA KUONDOKA UGANDA


Mbunge wa Uganda ambaye inadaiwa aliteswa na maafisa wa usalama,Robert Kyagulanyi maarufu kwa jina la Bobi Wine ameruhusiwa kusafiri kuelekea Marekani kwa ajili ya matibabu.

Alhamisi usiku Polisi walimkamata Kyagulanyi na mbunge mwenzake wa upinzani Francis Zaake uwanja wa ndege wa Kampala wakati wakijiandaa kwenda nje ya nchi kupatiwa matibabu.

Polisi walidai kuwa viongozi hao wa upinzani, ambao wote wanakabiliwa na tuhuma za uhaini walikuwa katika harakati za kukimbia nchi.

Hata hivyo, wabunge hao wawili wamesema kuwa waliteswa baada ya kukamatwa huko nyuma na hospitali ya Kampala ilitoa pendekezo kwamba wapatiwe matibabu nje ya nchi.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.