MTOTO WA RAIS AGOMA KULA


Mtoto wa Rais wa zamani wa Angola, José Eduardo dos Santos, Mkurugenzi wa zamani wa mfuko wa kitaifa nchini humo, Jose-Filomeno dos Santos ambaye amewekwa rumande tangu wiki hii baada ya kutuhumiwa kwa makosa ya ubadhirifu na ulaji rushwa, ameanza mgomo wa kula.

Vyombo vya habari nchini humo vimekariri vyanzo kutoka jela na kunukuliwa na Shirika la Habari la AFP juu ya hatua ya mtoto huyo kukataa kula chochote akiwa rumande.

“Anakataa kula tangu Jumanne, familia yake inaleta chakula lakini hali,” moja ya vyanzo hivyo kimeliambia Shirika la Habari la AFP.

Jose-Filomeno dos Santos ambaye ni Mkurugenzi wa zamani wa Mfuko wa Kitaifa wa Angola, mwenye umri wa miaka 40, anazuiliwa katika Gereza la Sao Paulo kwa agizo la Ofisi Mwendesha Mashtaka mkuu wa Serikali ya nchi hiyo.

Aidha, Jose-Filomeno dos Santos anayefahamika kwa jina la Zenu, alifunguliwa mashtaka Machi mwaka huu kwa madai ya ufisadi, kujitajirisha kinyume cha sheria, kushirikiana na wahalifu na kuweza kupitisha mlango wa nyuma akiwa pamoja na washirika wake hadi dola biloni 1.5.

Amekuwa wa kwanza kutoka familia ya Rais wa zamani, Dos Santos kufungwa tangu mrithi wake, Joao Lourenço kuchukua hatamu ya uongozi wa nchi mwaka mmoja uliopita.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post