
Ombi hilo limetolewa na Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema.
“Wabunge wamekuwa wakiahidiwa kupewa ubunge wao baada ya kuhamia CCM, hiyo ni aina nyingine ya rushwa, Takukuru waingilie kati suala hilo na kuchukua hatua,” amesema.
Mrema alidai suala la wabunge na madiwani wa Chadema kutimukia CCM haliwapi shida kwa sababu wanajua mazingira yalivyo sasa.
Alidai Mbunge huyo (Ryoba) amefanya kile alichokisema wakati wa mkutano wa Rais Magufuli huko Serengeti na kwamba hawashangazwi na uamuzi wake kwa sababu yeye siyo wa kwanza kuhama.