WATU 90,000 KUPIMWA UKIMWI MANYARA



Na John Walter-Hanang

Katika kuendelea kuunga mkono jitihada za serikali kuimarisha huduma za Afya ikiwemo Ukimwi,Taasisi ya Benjamin Mkapa imekuja na mradi wa miaka mitatu ndani ya mkoa wa Manyara kuanzia June 2018 hadi Desemba 2020 wenye kufanya upimaji wa Ukimwi katika kata 46 za wilaya ya Mbulu na Simanjiro.

Aidha imeelezwa kwamba mpaka kukamilika kwa zoezi hilo katika wilaya hizo, Jumla ya watu 2081 kila kata wanatarajiwa kupimwa virusi vya Ukimwi na kupatiwa ushauri na Nasaha kwa wale watakaobainika kuwa na maambukizi na kuanza dawa haraka.

Katika uzinduzi huo uliofanyika mjini Katesh, mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Hanang Joseph Mkirikiti kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Manyara Alexender Mnyeti alisema ni muhimu kila mmoja kupima afya yake na kujitambua kwa maendeleo ya Taifa.

Dc Mkirikiti amesema “katika utekelezaji wa dhana hii tunazingatia dhana kuu ya utekelezaji wa tisini tatu,tisini ya kwanza inasema wale ambao wanapimwa na wamejua afya zao waanzishiwe dawa,tisini ya pili inasema wale ambao watakuwa tayari wameanshiwa dawa wazingatie matumizi ya dawa na tisini ya tatu inasema wale watakaokuwa tayari wameanza kutumia dawa basi wawe na virusi ambavyo vimedhibitiwa yaani ambayo haviongezeki”alisema Mkirikiti na kuongeza kuwa Tanzania Bila Ukimwi Inawezekana.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Furaha yangu,Pima,Jitambue,Ishi mhamasishaji wa Taasisi ya Benjamin Mkapa mkoa wa Manyara Dr. Daudi Ole Mkopi amesema katika zoezi hilo wanatarajia kupima jinsia zote japo changamoto inaonekana kwa kina Baba.

Hata hivyo tangu kuanza kwa zoezi hilo katika wilaya ya Hanang Agosti 25, 2018 ambapo mpaka Septemba 28 watu 1426 walijitokeza kupima maambukizi ya virusi kwa hiari 771 na wanawake 655 na kati yao wanaume watatu na wanawake wawili waligundulika kuwa na Virusi vya Ukimwi na kuunganishwa na huduma za matunzo na matibabu kwenye vituo vya karibu

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527