WATANO WAFARIKI KWA AJALI YA GARI DEREVA AKIKIMBIA ASKARI WA DORIA

Watu watano wamefariki dunia papo hapo na wengine watatu kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kutoka Busurwa mwambao wa Ziwa Victoria wilayani Rorya kwenda mjini Tarime kupinduka.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tarime na Rorya, Henry Mwaibambe amesema ajali hiyo ilitokea katika kitongoji cha Bukwe eneo la Mika alfajiri ya jana Agosti 14, 2018, ambapo uchunguzi wa awali umebaini chanzo cha ajali ni mwendo kasi uliosababishwa na dereva aliyekuwa akiwakimbia askari wa doria.

Kamanda Mwaibambe amesema dereva wa gari hilo aliyejulikana kwa jina la Athumani Masiaga ambaye ni miongoni mwa waliofariki dunia alikataa kutii amri ya kusimama iliyotolewa na askari wa usalama barabarani kutokana na kubeba samaki wanaosadikiwa kupatikana kutokana na uvuvi haramu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527