ASKARI MSTAAFU WA JWTZ MBARONI TUHUMA ZA KUKODISHA SILAHA KWA MAJAMBAZI

Askari mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) anashikiliawa na jeshi la polisi Mkoani Morogoro kwa tuhuma za kukodisha silaha kwa wahalifu zinazotumika kwenye matukio ya ujambazi.

Akizungumza jana Agosti 14, kamanda wa polisi mkoani Morogoro, Wilbroad Mutafungwa alisema watuhumiwa 39 wa matukio hayo walihusishwa kwenye matukio ya uhalifu ikiwamo kukutwa na silaha za aina tano, bangi kete 200, bangi misokoto 66, risasi 27, pamoja na pombe aina ya gongo lita 58.

Mtuhumiwa Lumi Guya maarufu kama Mbulu (67) mkazi wa Kingolwira alikamatwa kwa tuhuma za kukodisha silaha yake aina ya Shot Gun anayoimiliki kihalali kwa watu wanaofanya uhalifu.

Kamanda huyo amesema mtuhumiwa huyo ni mwanajeshi mstaafu wa JWTZ na hushirikiana na Miraji Jumanne(28)mkazi wa Kichangani ambaye inadaiwa aliwahi kuwa askari polisi na kufukuzwa kutokana na vitendo visivyofaa wakishirikiana na wenzao sita ambao wote wanashikiliwa.

Watuhumiwa wengine walikamatwa katika matukio ya wizi, uuzaji gongo, wafugaji kulisha mifugo kwenye mashamba ya wakulima na wizi wa kutumia silaha.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.