WAETHIOPIA 25 WAKAMATWA WAKIJARIBU KUPITA TANZANIA BILA KUFUATA SHERIA


Raia 25 wa Ethiopia waliokamatwa wakati wakijaribu kupita nchini bila ya kufuata Sheria wakishuka kwenye gari walipofikishwa kituo kikuu cha Polisi mjini Moshi.
Baadhi ya raia hao wa Ethiopia wakiwemo watoto tisa wenye umri chini ya miaka 18 wakiwa kituo kikuu cha Polisi mjini Moshi.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Hamis Issah akitoa taarifa juu y akukamatwa kwa raia 25 wa Ethiopia waliongia nchini bila ya kufuata Sheria.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini 

Jeshi la Polisi linawashikilia raia 25 wa Ethiopia miongoni mwao tisa ni watoto wenye umri chini ya miaka 18 wakiwa katika kichaka eneo la Himo wakisubiri gari kwa ajili ya kuwavusha kuendelea na safari yao ya Afrika Kusini.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Maidizi wa Polisi,Hamis Issah amesema raia hao wa Ethiopia walikamatwa na askari Polisi wakati wa doria wakiwa na kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la Baraka itema (25) aliyejitambulisha kama fundi ujenzi.

Raia hao 25 wa Ethiopia wanaendelea kuhojiwa na Idara ya Uhamiaji kwa kusaidiana na jshi la Polisi na kwamba mara baada ya taratibu kukamilika watafikishwa mbele ya vyombo vya sheria kujibu tuhuma zinazowakabili za kuingia nchini bila ya kibali.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527