Thursday, August 2, 2018

TIBA YA UKARABATI WA UKE INAWEZA KUSABABISHA HATARI KUBWA

  Malunde       Thursday, August 2, 2018
Wanawake wanaonywa dhidi ya hatari za mchakato wa kubadili umbo la uke ama kuurejesha katika hali yake asilia.

Wataalamu wanasema "matibabu", yanayotolewa na baadhi ya kliniki za kibinafsi katika mataifa mbali mbali yakiwemo ya Uingereza na Marekani yanaweza kumsababishia mwanamke kuungua vibaya, kupata makovu na kupata maumivu ya mara kwa mara.

Wakati wa matibabu haya, kifaa huingizwa ndani ya uke kwa ajili ya kuchemsha kukata nyama ya uke.

Ingawa matibabu haya si ya upasuaji na yanaweza kufanyika kwa muda mfupi tu, wataalamu wanashauri kuwa ni muhimu kuwa salama.

Matibabu hayo kwa njia ya vifaa vya kuchoma seli yameidhinishwa kwa matumizi ya matibabu ya kuua seli za saratani ya mfuko wa uzazi ama nyama ya uke pamoja na masundosundo ya sehemu za siri (genital warts) , lakini hayajafanyiwa vipimo vya ukarabati wa mwili

Mamlaka ya viwango vya bidhaa nchini Marekani SDA inasema kuwa itachukua hatua ikiwa wenye kuuza "tiba hatari isiyo na dhihirisho la faida " wataendelea kufanya hivyo.

Inasema wengi miongoni wa waotengenezaji bidhaa hizo wamekuwa wakidai tiba hiyo inaweza kuponya maradhi na dalili zinazosababishwa na kipindi cha ukomo wa kupata mtoto (menopause), uwezo wa kudhibiti mkojo na uwezo wa kufanya tendo la ngono.

"Bidhaa hizi zina hatari kubwa na hazina ushahidi wowote wa kuithibitisha ushahidi wa matumizi yake. Tuna wasi wasi mkubwa wanawake wanadhurika ," linasema onyo la FDA.

Paul Banwell, daktari wa upasuaji wa kurekebisha maumbile ya mwili na mjumbe wa Jumuiya ya madaktari wa upasuaji wa kurekebisha mwili wanaokubalika alisisitizia onyo la FDA: "Kumekuwa na ongezeko kubwa la haja ya afya ya wanawake na maslahi ya kingono, pamoja na kwamba hili linapaswa kuungwa mkono, ni muhimu kwamba elimu yoyote na tiba vinavyotolewa vitolewe kwa umakini bila kuwepo upotoshaji au uchochezi wa masoko ."

Dkt Vanessa Mackay, kutoka chuo cha Uingereza za madaktari bingwa wa masuala ya uzazi cha Royal College of Obstetricians and Gynaecologists (RCOG), amesema: "Hakuna ushahidi unaoonyesha kwamba vifaa vya ukarabati wa uke usiotumia vifaa unafaa katika kuboresha misuli ya uke ama kubadili muundo wa uke . Kama wanawake wanahofu juu ya muonekano ama mguzo wa uke wao wanapaswa kuongea na wataalamu wa afya wenye taaluma''

Ni muhimu kukumbuka ,hata hivyo, kwamba kila mwanamke ana uke tofauti . Uke wa mwanamke mmoja na tofauti na wa mwanamke mwinginekama wanavyotofautiana wanawake wenyewe katika muonekano wao wa sura na rangi, wanasema wataalamu.
Dkt Vanessa anasema: " Ili kuimarisha misuli inayozingira uke wanawake wanashauriwa kujaribu mazoezi ya sehemu ya chini ya tumbo (pelvic) ya sakafuni yanayoweza kusaidia kuboresha na kuimarisha misuli na uwezo wa kupata shauku ya ngono'."

Namna ya kufanya mazoezi ya sehemu ya chini ya kiuno (pelvic):
Keti au usimame wima huku magoti yako yakiwa yameachana kidogo na kisha pandisha juu misuli ya sehemu ya chini ya kiuno kama unataka kuzuwia kupitisha mkojo.
Ni muhimu kutokaza tumbo, makalio au misuli ya mapaja wakati wa mazoezi haya.

Fanya mazoezi 10 ya kubana na kuachilia misuli kwa sekunde 10 hivi kwa kila awamu.

Urefu wa muda wa kukaza misuli unaweza kuongezwa kadri unavyo endelea na na kuiachilia taratibu halafu unaweza kuendelea kwa kukaza misuli hiyo kwa haraka.

Ukavu wa uke ni jambo la kawaida lakini ni tatizo linaloweza kutibiwa ambalo wanawake wengi wanalipitia wakati mmoja maishani mwao.

Unaweza usababishwa na mambo kadhaa ikiwemo kufukia kipindi cha ukomo wa kujifungua menopause, kunyonyesha, uzazi , kutopata shauku kabla ya ngono na baadhi ya dawa za kuzuwia mimba.

Wanawake wanashauriwa kujaribu kujisaidia wenyewe kabla ya kuwatembelea wataalamu wa afya, ikiwemo kutumia vilainishi vya uke .

Na kama tatizo litaendelea , daktari anaweza kumpatia dawa ya vichocheo vya mwili (hormone) kwa ajili ya uke inayofahamika kama oestrogen, inasema taasisi ya RCOG.
Chanzo-BBC
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post