SERIKALI YATAHAMAKI SARUJI KUADIMIKA MTAANI

Serikali imekutana na wadau wa sekta ya viwanda kujadili kuadimika kwa saruji, huku inayopatikana ikiuzwa bei ya juu.

Kikao hicho kilichoongozwa na Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Stella Manyanya kilihudhuriwa na wazalishaji wa saruji na wa makaa ya mawe, wasafirishaji na wadhibiti.

Akizungumza katika mkutano huo Manyanya amewataka wazalishaji wa saruji kueleza uwezo wao wa uzalishaji.

Naibu waziri pia amewataka kueleza sababu za kusimamisha uzalishaji ghafla na kwa viwanda vyote.

"Imetushitua kuona saruji imepotea sokoni na kupanda bei ghafla, tena viwanda vyote. Tukasema hapo ni zaidi ya masuala ya kiufundi, kwa hiyo tumewaita kuwasikiliza tujue tatizo ni nini ikiwezekana leo tutoke na uamuzi,” alisema Manyanya.

Alisema sasa kuna fursa nyingi za soko la saruji kupitia miradi inayotekelezwa na Serikali na kwamba hiki ndicho kipindi cha kuongeza uzalishaji lakini anashangazwa kuona saruji imeadimika na bei imepanda.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.