MTANZANIA ACHAGULIWA KUWA MBUNGE PAKISTAN


Tanzeela Qambrani mbunge wa Jimbo la Sindh nchini Pakistan.

Mwanamke mmoja aitwaye Tanzeela Qambrani ambaye asili yake ni Tanzania ameandika historia kuwa Mwafrika wa kwanza kuchaguliwa kuwa mbunge katika Jimbo la Sindh nchini Pakistan akiwakilisha wanawake.

Tanzeela ambaye anatoka jamii inayodharauliwa ya waliowachache ya Sheedi yaani watu wenye asili ya Afrika, aliapishwa Jumatatu kuwa mjumbe wa Bunge la Sindh kupitia chama cha Pakistan People’s Party (PPP).

Inaelezwa kuwa Tanzeela ambae amekuwa mtetezi wa elimu na haki za wasichana nchini humo ametokea kwenye jamii Sindh ambayo ndio jamii ya watu wenye asili ya Afrika ambao hubaguliwa sana nchini humo.

Baada ya kuapishwa amesema “Nimejihisi kama Nelson Mandela wakati naapishwa naamini nitakwenda kuipa heshima jamii yangu ambayo imejitahidi kulinda tamaduni za kiafrika licha ya kuwa kwenye himaya ya watu weupe”.

Inadaiwa kuwa Mababu wa Tanzeela ambae ni mtaalamu wa masuala ya Kompyuta walitokea Tanzania kabla ya kuingia nchini humo huku Dada yake mmoja na Tanzeela anatajwa kuolewa nchini Tanzania.

Aidha Tanzeela ana matumaini kuwa uteuzi wake utasaidia kuondoa unyanyapaa na ubaguzi dhidi ya Watu wa jamii yake ya Sidi wenye asili ya Afrika.

Mpaka sasa familia ya Tanzeela imeendelea kuweka muunganiko na Afrika kwani mmoja wa dada zake aliolewa Tanzania, wakati mwingine aliolewa Ghana.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527