RC GAGUTI AWEKA JIWE LA MSINGI NA KUZINDUA UJENZI WA BARABARA MANISPAA YA BUKOBA | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, August 23, 2018

RC GAGUTI AWEKA JIWE LA MSINGI NA KUZINDUA UJENZI WA BARABARA MANISPAA YA BUKOBA

  Malunde       Thursday, August 23, 2018

Mkuu wa mkoa wa Kagera brigedia Jenerali Marco Gaguti ameweka jiwe la msingi katika moja ya barabara na kuzindua ujenzi barabara nne zenye urefu wa kilometa tano zinazojengwa katika Manispaa ya Bukoba na Serikali ya Tanzania kwa ufadhili wa benki ya Dunia kwa gharama ya shilingi bilioni 7.


Katika uzinduzi huo ulifanyika leo katika kata ya Nshambya Manispaa ya Bukoba Gaguti aliwataka wananchi kuwa walinzi wa miradi kama hiyo inayotekelezwa kwa fedha nyingi ya Serikali ambazo pia zimo kodi za wananchi hao zinazotokana na kazi wanazofanya kutokana na kipato halali.


Alisema kuwa uwekezaji huo mkubwa ambao umefanywa na Serikali ya awamu ya tano katika kuboresha miundombinu ya usafiri na usafirishaji hivyo serikali inaendelea kuwekeza katika kuwaletea maendeleo ya haraka wananchi wake wakiwemo wa mkoa huo katika sekta ya miundombinu.

Pia alimwagiza mkandarasi anayejenga mradi huo kujenga kwa viwango vilivyokusudiwa na muda uliopangwa kwani utachangia ukuaji wa uchumi kwa wananchi na kurahisisha usafiri na usafirishaji kwao katika na ustawi wa jamii hiyo.

“Mradi huu upo kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu na wananchi wetu kwa ujumla,kwangu mimi itakuwa ni furaha kubwa endapo mradi utaisha kabla ya muda kwani, dhambi ni kuchelewa kukamilisha na kama kutakuiwa na vikwazo ndani ya mkoa tuko tiyali kushirikiana kuviondoa ili wananchi waweze kufaidi manufaa ya uwekezaji wa Serikali yao”alisema Gaguti.

Alisema kila mmoja ni mdau katika miradi ya maendeleo hivyo akawaeleza wananchi kwamba miradi inayotekelezwa na Serikali hata wao inawagusa hivyo pale wanapoona hujuma katika miradi basi watoe taarifa mapema kuliko kusubiri mambo yakaharibika na kuingizia Serikali hasara wakati wao walikuwa wakiona.

Akitoa taarifa ya mradi mwahandisi Andondile Mwakitaru mratibu wa mradi ambaye pia ni meneja wa wakala wa barabara vijijini (TARURA) Manispaa hiyo alisema kuwa Manispaa ya Bukoba ni moja ya miji 18 ya Tanzania ambayo imepangiwa fedha na Serikali kupitia ufadhili wa banki ya dunia kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali.

Mwakitaru alisema miradi hiyo inatekelezwa chini ya progamu ya uimarishaji miji pamoja na shughuli nyingine zilizopangwa kufanyika chini ya mpango huo hivyo Manispaa yao inajenga barabara nne kwa kiwango cha lami nzito.

Alizitaja barabara hizo kuwa ni Nshambya Km.1.7 ambayo imewekewa jiwe la msingi,Nyangoye –Halmashauri ya Bukoba km 1.3,barabara ya Shoo km 1.05 na Binsaidi- Kilimahewa km 0.95 ambapo ujenzi wa mradi huo unafanywa na mkandarasi NCL International ltd wa jijini Dar es Salaam ambapo zote ujenzi wake unaendelea.

Alisema kuwa mkataba wa kazi hiyo ni wa miezi kumi ambapo umeanza kutekeleza Juni 18 mwaka huu na unatarajiwa kukamilika Aprili 17 ,2019 ambapo mradi huo unajengwa kwa usimamizi wa mhandisi mshauri Advance Enginering Solution Ltd ya jijini Dar esa Salaam.
Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera brigedia jenerali Marco Elisha Gaguti akikagua mradi wa ujenzi wa barabara ya kilometa 1.7 inayojengwa katika eneo la Nshambya Manispaa ya Bukoba ambayo ni kati ya barabara nne za Manispaa hiyo, zitakazojengwa kwa kiwango cha lami nzito kwa gharama ya shilingi bilioni 7 kutoka banki ya dunia.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post