CUF YA LIPUMBA YAUNGANA NA CHADEMA


Chama cha Wananchi (CUF) kimeshangazwa na nguvu inayotumika kuwazuia wapinzani kushiriki uchaguzi katika Jimbo la Korogwe Vijijini, licha ya eneo hilo kuwa ngome ya CCM.

Mkurugenzi wa habari na mawasiliano kwa umma wa CUF, Abdul Kambaya ambaye yupo upande wa CUF inayoongozwa na mwenyekiti anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba, amesema, kitendo cha wapinzani kuzuiwa kurudisha fomu katika jimbo hilo ambalo mbunge aliyepita alikuwa anakubalika, ni wazi Serikali haijiamini.

"Chama cha wananchi CUF kinapinga kauli ya mkurugenzi wa uchaguzi, Dkt. Athuman Kihamia kuwa wagombea wa upinzani walirejesha fomu katika ofisi zisizo sahihi", amesema Kambaya.

Hayo yamejiri baada ya msimamizi wa uchaguzi katika jimbo hilo ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Korogwe, Dkt. George Nyaronga kutangaza kuwa mgombea wa CCM ambaye ni Timotheo Mzava amepita bila kupingwa baada ya muda wa mwisho wa kurejesha fomu Agosti 20, 2018 saa 10 jioni kuwa peke yake, hali iliyopelekea .

Jimbo la Korogwe Vijijini limekuwa wazi kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Stephen Ngonyani maarufu kama Maji Marefu.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.