Wednesday, August 1, 2018

RAIS MAGUFULI AWAAPISHA VIONGOZI ALIOWATEUA..ASEMA ILIMLAZIMU KUKAA NA MAJINA YAO MIEZI MINNE AKIWACHUJA

  Malunde       Wednesday, August 1, 2018
Rais John Magufuli, amewaambia Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala na Makatibu Wakuu alikaa na majina yao kwa muda wa miezi mine kabla ya kuwateua kushika nafasi hizo.


Akizungumza baada ya kuwaapisha viongozi hao leo Jumatano Agosti Mosi, Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli pia amewataka viongozi hao kutambua ni Mungu ndiye amewachagua.


“Nimekaa na majina yenu zaidi ya miezi minne, wengine wamepungua wengine wameongezeka.


“Tanzania ni kubwa mno, mimi sikufaa kuwa rais, ni Mungu alitaka na ndiyo sababu siwezi nikasimamam nikajisifu, ni Mungu alitaka vile vile Makamu wa Rais.


“Hata Waziri Mkuu… kwanza hata sijui nilimchaguaje, kwa sababu kuna watu walikwenda Dodoma na suti wameshona ili wawe Waziri Mkuu, lakini Majaliwa (Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa) ni Mungu aliamua awe Waziri Mkuu, vivyo hivyo katika nafasi zenu,” amesema Rais Magufuli.


Aidha, Rais Magufuli pia amesema nafasi hizo kwa viongozi hao, zimepangwa na Mungu ambaye alitaka wazipate ambapo wakiamini hivyo kila mmoja katika nafasi yake atatenda haki kwa wakati wake.


“Wengine wanasema nimechagua wapinzani, nani mpinzani Tanzania hii, Kafulila (David Kafulila, Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe) mtasema ni mpinzani.


“Alipokuwa huko alipigania suala la IPTL, akaitwa tumbili leo umteue useme umeteua mpinzani, huyu si mpinzani ni mpiganaji wa serikali yake,” amesema.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post