MZEE MAJUTO KUZIKWA SHAMBANI KWAKE TANGA LEO


Mwili wa aliyekuwa msanii gwiji wa filamu nchini, Amri Athumani ‘King Majuto’, unatarajiwa kuzikwa leo mkoani Tanga katika shamba lake lililopo katika kijiji cha Kiruku ambako maeneo ya Donge ambako viongozi mbalimbali wa serikali, akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela, wamefika kushiriki maziko yake.

Mzee Majuto alifariki usiku wa Jumatano, Agosti 8, 2018 katika Hospitali ya Muhimbili, ambapo kesho yake, Agosti 9, 2018 mwili wake ulipelekwa katika Msikiti wa Maamur, Upanga, jijini Dar es Salaam, kuswaliwa kabla ya kupelekwa viwanja vya ukumbi wa Karimjee kuagwa.

Mwili wa muigizaji wa vichekesho Amri Athumani 'Mzee Majuto' umewasili Donge nyumbani kwake usiku wa kuamkia leo majira ya 7.05 usiku .

Safari ya kwenda Tanga kwa ajili ya mazishi ilianza saa 10.15 jioni baada ya kumuaga katika ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam.

Leo Agosti 10,2018 kuanzia saa 5.45 mchana, ibada ya mazishi itafanyika katika msikiti wa Nuruguda uliopo karibu na nyumbani kwake na kuzikwa kijiji cha Kiruku yalipo mashamba yake nje kidogo cha jiji la Tanga.

Mzee Majuto alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya Tezi Dume ambapo Januari mwaka huu,alifanyiwa upasuaji katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es Salaam na kisha baadaye kupelekwa India kwa Matibabu zaidi . June 23, mwaka huu alirejea nchini na kupelekwa moja kwa moja katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Marehemu ameacha mjane na watoto kumi.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.