STEVE NYERERE,CLOUD WAZUA JAMBO MSIBANI KWA MZEE MAJUTO TANGA...FAMILIA YASHANGAA | MALUNDE 1 BLOG

Friday, August 10, 2018

STEVE NYERERE,CLOUD WAZUA JAMBO MSIBANI KWA MZEE MAJUTO TANGA...FAMILIA YASHANGAA

  Malunde       Friday, August 10, 2018
Baada ya mwili wa Mzee Majuto kuwasili nyumbani kwake Mtaa wa Donge katika jiji la Tanga, ilizuka sintofahamu baada ya wasanii wakiongozwa na Steve Nyerere na Cloud 112 kufanya jambo ambalo familia haikupendezwa nalo.


Tukio hilo lilizua kutoelewana kati ya wasanii waliotoka Dar es Salaam na wenyeji wa eneo hilo, baada ya wasanii hao walipofika kuingia ndani na kusema wanaenda kukagua sehemu ya kuhifadhiwa mwili.


Wenyeji waliona kama wamedharauliwa na kuwauliza ina maana sisi hamtuamini hadi kufikia hatua ya kukagua sehemu ya kuhifadhi mwili?


Miongoni mwa wasanii waliodai sehemu ikaguliwe ni Steve Nyerere na Cloud ambao waliwaita askari waliovaa kiraia na kuingia nao ndani.


Mzozo huo ulisababisha mwili utolewe kwa fujo kwenye gari ya kubebea wagonjwa, huku watu wakisukumwa na baadae mlango wa nyumba ya Majuto ukafungwa na watu wakaambiwa wasubiri nje.


Baadhi ya wasanii walifika Tanga kwa ajili ya mazishi ni JB, Steve Nyerere, Baba Haji, Shamsa Food, Muhogo Mchungu, Simon Mwakifamba ambaye ni Rais wa Shirikisho la filamu na wasanii wengine walikuwa wametangulia ambao ni Riyama, Nisha, Hamornize na wengine wengi.
Na Rhobi Chacha, Mwananchi
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post