MWALIMU AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUBAKA MWANAFUNZI

Mwalimu wa Shule ya Sekondari Engusero wilayani Kiteto, mkoani Manyara, Henry Michael (30), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kiteto kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wa Kidato cha pili (16).


Mwendesha mashtaka wa polisi, Inspekta Mbaruku Makame, amedai mahakamani hapo leo Jumatano Agosti 29, kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 26, mwaka huu saa mbili usiku shuleni hapo baada ya mwanafunzi huyo kutumwa baadhi ya vifaa nyumbani kwa mtuhumiwa huyo.


Amedai mwanafunzi huyo alikuwa anaishi bweni na wenzake ambapo usiku wa siku hiyo mtuhumiwa huyo alimtuma aende nyumbani kwake kuchukua vifaa vya shule ndipo akamfuata nyuma na kumbaka kichakani.


Baada ya kusomewa shitaka hilo mshtakiwa amekana na kurejeshwa rumande kwa kushindwa kutimiza msharti ya dhamana yaliyotaka kuwa na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya Sh milioni mbili na kesi imeahirishwa hadi Septemba 5, mwaka huu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post