MAMIA WAJITOKEZA KUAGA MWILI WA MZEE MAJUTO DAR

Mamia ya waombolezaji wamejitokeza katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam kuaga mwili wa aliyekuwa muigizaji nguli wa vichekesho nchini, Amri Athumani ‘Mzee Majuto’ leo Agost 9, 2018.


Mzee King Majuto alifariki dunia jana majira ya saa 2:00 usiku Agosti 8, 2018 katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu kwa siku kadhaa.


Baada ya kuaga mwili utasafirishwa kwenda nyumbani kwake jijini Tanga kwa maziko ambayo yatafanyika kesho Ijumaa.

Tazama Video hapo chini




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527