MKAPA MGENI RASMI KESHO MAADHIMISHO KILELE NANENANE KITAIFA MKOANI SIMIYU | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, August 7, 2018

MKAPA MGENI RASMI KESHO MAADHIMISHO KILELE NANENANE KITAIFA MKOANI SIMIYU

  Malunde       Tuesday, August 7, 2018
Na Stella Kalinga, Simiyu
RAIS mstaafu Mhe. Benjamini Mkapa kesho Agosti 08, atakuwa Mgen Rasmi katika Kilele cha Maonesho ya Sherehe ya wakulima Nanenane Kitaifa mwaka 2018, ambayo yanafanyika katika Uwanja wa Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.


Akizungumza na vyombo vya habari , Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema Mkapa atakuwa mgeni rasmi katika madhimisho hayo akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. 


Amesema pia katika kilele cha Maadhimisho ya maonesho hayo viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali watashiriki wakiwemo Katibu Mkuu wa CCM , Dkt. Bashiru Ally Sambamba na Mawaziri, Manaibu Waziri na Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Mkuu wa wizara mbalimbali.


“Watakuwepo viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali pamoja na viongozi wa Taasisi mbalimbali za Fedha wakiwemo Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania(BOT) Prof. Florens Luoga na Mkurugenzi wa Benki ya NBC, Theobald Sabi”


“Wageni wengine ni Wakurugenzi wa Benki ya NBC na NMB pamoja Viongozi waandamizi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, hivyo napenda kuwakaribisha wananchi wote wa Mikoa ya Mara, Shinyanga na kwa msisitizo wananchi wa Simiyu ambao ndiyo mkoa mwenyeji kujitokeza kwa wingi kushuhudia maadhimisho ya maonesho haya ambayo ni mara ya kwanza kufanyika Mkoani kwetu” alisema.


Katika hatua nyingine Mtaka amewahakikishia wananchi kuwa usafiri wa kufika katika Uwanja wa Nanenane utakuwa wa uhakika kwa kuwa mabasi ya kwenda huko yapo ya kutosha na nauli zimepunguzwa kutoka Lamadi mpaka Nyakabindi na kutoka Mjini Bariadi kwenda Nyakabindi.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post