MELI YA MIZIGO YAWAKA MOTO BAGAMOYO | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, August 14, 2018

MELI YA MIZIGO YAWAKA MOTO BAGAMOYO

  Malunde       Tuesday, August 14, 2018

Mfano wa picha ikionesha Meli ikiwaka moto.

Meli ya mizigo ijulikanayo kama LCT Rahimu imewaka moto mapema leo ikiwa katika bandari ya Bagamoyo.

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo, Fatuma Latu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kutaja chanzo chake kuwa ni hitilafu ya umeme wakati mafundi wakijaribu kuchomelea mlango wa meli hiyo kwa kutumia umeme wa jenereta iliyokuwa ndani yake.

Amesema vyombo vya zimamoto na uokoaji vimefanikiwa kuzima moto huo na kwamba nahodha kwa sasa anahojiwa na vyombo vya usalama ili kupata maelezo zaidi.

Inadaiwa kuwa meli hiyo imetokea visiwani Zanzibar na ilikuwa bandarini hapo ikisubiri shehena ya kokoto kwa ajili ya kuipeleka Zanzibar.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post