MBUNGE WA CHADEMA AKANUSHA TAARIFA ZA KUHAMIA CCM

Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini (CHADEMA), Anthony Komu amekanusha kauli iliyotolewa na aliyekuwa Mbunge wa Ukonga (CHADEMA) kuwa mbunge huyo yuko mbioni kutimkia CCM.


Komu amesema kuwa hawezi kuondoka CHADEMA na hajawahi kufanya mazungumzo na Waitara kuhusu suala hilo kwani yeye ndio muasisi wa upinzani na anajivunia historia hiyo .


“Mimi sio sehemu ya mpango huo na sielewi Waitara katoa wapi taarifa hiyo naomba wananchi wangu watambue kuwa mimi sio mpinzani wa kuunga unga mimi ni miongoni mwa waasisi wa upinzani”, amesema Komu.


Jumamosi ya Agosti 11, 2018 wakati akiongea na kituo cha EATV, Waitara aliwataja wabunge watano kutoka CHADEMA wanaotaraji kujiunga na CCM akiwemo Anthony Komu.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.