MBUNGE WA CUF NAYE AHAMIA CCM


Mbunge mwingine toka Chama cha Wananchi CUF jimbo la Liwale,Zuberi Kuchauka kwa hiari yake mwenyewe ameamua kujivua uanachama wa chama hicho na kujiunga na Chama cha Mapinduzi CCM

Ametangaza uamuzi huo leo August 12, 2018 katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini Dar es Salaam, akiwa sambamba na Katibu Mkuu wa chama hicho tawala, Dk Bashiru Ally.

Kuchauka amesema moja ya sababu iliyomuondoa CUF ni utendaji kazi wa Rais John Magufuli pamoja na mgogoro unaokitafuta CUF.

Katibu Mkuu CCM, Dr. Bashiru amesema CCM itaendelea kupokea wanachama wapya na wanaorejea CCM.
Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally akizungumza mda mfupi kabla ya aliyekuwa Mbunge wa CUF katika jimbo la Liwale mkoani Lindi Zuberi Kuchauka (kulia), kutangaza kukihama Chama cha Civic United (CUF), na kujiunga na CCM, leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole.
Aliyekuwa Mbunge wa CUF katika jimbo la Liwale mkoani Lindi, Zuberi Kuchauka (katikati), akitangaza kukihama Chama cha Civic United (CUF), na kujiunga na CCM, leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally na kulia ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.